25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Asasi za kiraia zina jukumu la kusaidia kuondoa umaskini- Kiwanga

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MKURUGENZI Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS), Francis Kiwanga amesema Asasi za kiraia zinajukumu la kuisaidia kuondoa umaskini katika jamii pamoja kuona umuhimu wa maendeleo ya watu na sio vitu.

Akizungumza leo Jumatatu Oktoba 25, 2021 jijini Dodoma kwenye mjadala kuhusu nini mchango wa Asasi za kiraia kwa jamii pamoja na utoaji mchango wa Msaada wa kisheria kwa jamii katika wiki ya AZAKI inayoendelea Jijini Dodoma, Mkurugenzi huo amesema asasi za kiraia zinajukumu la kuisaidia kuondoa umaskini ulipo katika jamii.

Mkurugenzi huyo amesema umuhimu wa asasi hizo utaonekana kwenye jamii ikiwa  zitapambana  kuchochea  maendeleo ya watu na siyo vitu kwani tafsiri ya  maendeleo inaanza na watu  na sio vitu pekee. 

“Hakuna Maendeleo kama  watu wetu bado ni masikini,tunataka kuona watu wanaishi maisha ya uhakika, tunataka kuona watoto wanapata elimu nzuri ,afya na maji safi hiyo ndiyo mizania ya Maendeleo.

“Tunatamani kuona jamii inaondokana na umaskini kwanza ndipo maendeleo yanaonekana,azaki zinatakiwa kuona umuhimu wa maendeleo ya watu na siyo vitu.

“Tunaweza tukawa na majengo mazuri ya zahanati na vituo vya afya lakini watu wakiwa masikini watashindwa kufuta zile huduma Kwa kuwa hawana uwezo wa kugharamia huduma,”amesema na kuongeza;

“Nataka kuwapa mfano kuna wakati nilikuwa nasafiri kutoka Bukoba kwenda Mwanza kwa basi lakini nilikutana na masoko mazuri cha kushangaza hayakuwa na watu,watafanyaje biashara wakati hawana uwezo huo,! sasa tusijivunie namba za vitu bali maendeleo ya watu,” amesema Kiwanga.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga amesema Serikali inawekeza  lakini miradi mingi   haidumu kutokana na  wananchi wengi kutokuwa na  mwamko wa maendeleo sababu zikiwa ni   dhana ya umaskini inayowakabili.

Amesema ,wananchi wasipokuwa na uwezo hawawezi kutambua thamani ya miradi na hivyo kushindwa kuitunza

“Tunapaswa kutumia muda wetu mwingi kuwaelewesha Wananchi kuhusu maana ya maendeleo na umuhimu wake ili nao wapate kushiriki ujenzi wa maendeleo kwa vitendo,”ameeleza.

Henga ameeleza kuwa umaskini usipo tibiwa utaendelea kuwa kidonda kwa jamii ambapo  karibu asilimia 50 ya watoto waishio mitaani wanatokana  na ndoa zilizovunjika kutokana na ugumu wa maisha.

“Tunataka kupambana na umaskini uliopitiliza,tunasaidia   jamii  msaada wa kisheria pale wanapokuwa wamekwama na wakati mwingine kukosa uwezo wa kumpata wakili Kwa kukosa fedha,hivyo ndivyo tunapambana walau kuiokoa jamii”amefafanua.

Henga ametolea mfano wa  mwanamke ambaye alitumia muda wa miaka 40 kufuatilia mgogoro wa shamba lakini baada ya yeye kuingilia kati aliweza kufanikiwa kupata haki yake ya shamba kwa muda mfupi.

“Kesi nyingi zinatumia muda mwingi nyingine zinakuwa na mazingira ya rushwa,Lazima tuokatae rushwa ,rushwa ni umaskini, tunatamani. Kila mwananchi aelewe haki zake kisheria na hii itasaidia kuleta maendeleo na kumaliza kero ya kesi ndogo za kawaida kabisa zilizokuwa zikichukua miaka 2 hadi 4 kumalizika haraka,”amesema.

Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa Huru la Kilimo Nchini( ANSAF), Audax Rukonge akichangia katika mjadala huo  amesema, ili asasi ziweze kufanya vizuri ni lazima zijenge utamaduni wa kuwa na maono ya pamoja,vipaumbele,utekelezaji  na kuwa na mifumo ya uwajibikaji wa  pamoja.

Amesema asasi hizo   zinatakiwa kujenga tabia ya kuaminiana ili kuleta mashirikiano pamoja na kuwa na mawazo ya pamoja na kuwa na uwazi kwa kile wanachokifanya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles