24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati Kuu CCM yampitisha Dk. Tulia kugombea Uspika wa Bunge

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa imepitisha jina la Dk.Tulia Ackson Mwansasu kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 20, 2022 jijini Dodoma na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka wakati akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao maalum ambacho kiliketi mapema leo chini ya Mwenyekiti wake, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema kwa mujibu wa Katiba ya CCM, kikao hicho ni kwa mujibu wa taratibu za Katiba ya Chama kilikuwa kinatathmini utendaji wa Serikali zote mbili na kimejadili mambo mbalimbali ikiwemo majina ya wanaowania nafasi ya Uspika na kumteua Dk.Tulia kugombea nafasi hiyo.

Katika hatua nyingine Kamati hiyo imempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa katika utendaji wake wa kazi kwakuhakikisha wanafunzi wote nchini wameingia kidato cha kwanza kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa madarasa huku kikimpongeza Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kutokana na utendaji wake kwa kusimamia uchumi wa bluu.

Mchakato wa uchukuaji fomu za kuwania nafasi ya Spika wa Bunge ulianza rasmi Januari 10 hadi 15, 2022 kufuatia aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo Januari 6, Mwaka huu ambapo jumla ya wanachama 71 walijitokeza kuchukua na kurejesha fomu hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles