26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

CCM Ileje waiunga mkono Kamati Kuu kumpitisha Dk. Tulia

Na Denis Sinkonde, Songwe

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Ileje mkoani Songwe wameunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kumteua Dk. Tulia Ackson kugombea nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwenyekiti wa CCM wilayani Ileje, Hebron Kibona amesema hayo leo Ijumaa Januari 21, 2022 wakati wa mkutano wa halmashauri kuu ya chama hicho uliofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo Itumba.

Kibona amesema mchakato wa kumpata mgombea mmoja kati ya wagombea 71 walioomba nafasi ya kuteuliwa na chama kuwania nafasi ya Uspika kuongoza muhimili huo wa Serikali umekidhi vigezo hivyo kama wajumbe wa halmashauri kuu wilaya wanaunga mkono juhudi za kamati kuu ya CCM Taifa ikiongozwa na mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan.

“Kila mwana-CCM aliyechukua fomu kuomba kuteuliwa na chama kuwania nafasi ya Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa na sifa lakini chama kikaona kwa wakati huu anayepaswa kushika wadhfa huo ni Dk.Tulia ambaye ni Naibu Spika wa bunge na mbunge jimbo la Mbeya Mjini ambaye anapaswa kuungwa mkono,” amesema Kibona.

Katibu wa chama hicho Hassan Lyamba amesema mchakato wa vikao vya Sekeritalieti na halmashauri ya kamati kuu Taifa kwa uamuzi walichofanya kwa kuteua jina la Dk. Tulia Ackison Mwasasu kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Uspika wa bunge wanauunga mkono.

“Hakuna mtu ambaye hafahamu uwezo wa Dk. Tulia Ackison kutokana na uzoefu wake kiongozi tangu ateuliwe kuwa mbunge kuanzia mwaka 2015-2020 na hatimaye kugombea ubunge jimbo la Mbeya mjini na kushinda mwaka 2020, hivyo wabunge wa CCM wampigie kura za ndio,” amesema Lyamba.

Mbunge wa jimbo la Ileje mkoani hapa, Mhandisi Godfrey Kasekenya.

Mbunge wa jimbo la Ileje mkoani hapa, Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema kama mbunge wa jimbo la Songwe ameipongeza kamati kuu kumteua, Dk. Tulia kuwania nafasi za Uspika kwani uzoefu wake katika nafasi ya Unaibu Spika utakuwa chachu ya kulitumikia bunge kwa lengo la kuwaletea Watanzania maendeleo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana UVCCM Ileje, Maon Mbuba amesema mchakato uliotumika kumpata mgombea umekidhi vigezo kwa kuepusha rushwa kama ilivyozoeleka kipindi cha kumpata mgombea kupitia chaguzi mbalimbali.

Kwa kauli moja wajumbe wa kikao hicho wamekubaliana na maamuzi ya kamati kuu chini ya Mwenyekiti Samia Suluhu kupitia vikao vyote na kufanikisha kukonga mioyo ya Watanzania na wana-CCM wa Ileje kumpata Dk. Tulia Ackison.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles