26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Ghati apongezwa maandalizi miaka 45 ya CCM

Na Shomari Binda,Musoma

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara kimempongeza Mbunge Ghati Zephania, kwa kuwa mstari wa mbele kuchangia mahitaji ya maandalizi kuelekea maadhimidho ya miaka 45 ya chama hicho.

Akizungumza kwenye kikao kilichowashirikisha makatibu wa CCM Wilaya na wabunge, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Samwel Kiboye amesema sherehe za miaka 45 ya chama hicho ambazo kitaifa zinafanyika mkoani humo ni muhimu kila mwanachama kushiriki maandalizi yake.

Amesema Ghati ambaye ni Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mara, ameanza kwa kuchangia mchele, maharage pamoja na mafuta kwa ajili ya kupikia chakula cha watoto wanaojifunza alaiki ya tukio hilo na kudai kila mmoja anapaswa kushiriki.

Kiboye maarufu kwa jina la Namba Tatu, amesema sherehe za miaka 45 ya CCM ni kubwa na mkoa wa Mara umepewa heshima ya kuziandaa hivyo ni muhimu kushirikiana kwenye maandalizi yake.

Amesema licha ya maandalizi katika eneo hilo la alaiki ya watoto yapo maandalizi katika maeneo mengine ambayo yanahitaji michango mbalimbali.

“Nimshukuru mbunge Ghati kwa moyo wake wa kuchangia na kwa kuanza kwa hivyo alivyotoa lakini tukumbuke hizi sherehe ni zetu na kila mmoja ashiriki kwenye maandalizi yake.

“Yupo mjumbe wa Baraza la Wanawake Taifa (UWT), Rhobi Samwel naye amechangia kwenye eneo hilo niwashukuru na muendelee na moyo huo kama wanachama lakini kama viongozi,” amesema Kiboye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles