MIONGONI mwa wasanii ambao wameÂtokea kukubalika katika miondoko ya Hip Hop ni Jeremiah KALA Masanja ‘Kala Jeremiah’ambaye anasumbua mbaya na ngoma zake kali zenye mashairi ya kiharakati.
Staa huyu ambaye ni zao la shindano la Bongo Star Search (BSS), msimu wa kwanza – mwaka 2007, anatamba na nyimbo kama Walewale, Wimbo wa Taifa, Waambieni na nyinginezo zikiwa zimetoa ujumbe mzuri kwa jamii na hasa kuwaÂkumbusha wanasiasa ahadi walizotoa kwa wananchi wao.
Katika mahojiano na Swaggaz yaliyofanyika wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam, Kala amezungumza mengi kuhusiana na maisha yake kabla, ndani na nje ya sanaa.
Pamoja na mengine mengi, Kala alitoa maoni yake kuhusiana na wasanii wanaoÂzalishwa na shindano la Bongo Star Search (shindano lililomtoa), kupotea muda mfupi baada ya kutangazwa washindi.
Akizungumzia hilo, alisema: “Siyo wote wanapotea. Mfano mimi nilikuwa mshindi wa nne kwenye shindano hilo mwaka 2007. Nipo na ninafanya vizuri. Yupo Peter Msechu na wengineo, kwahiyo siyo wote.
“Lakini angalau naweza nikawazunÂgumzia hao ambao wanaobuka washindi halafu wanapotea. Hii inatokana na baadhi yao kuimba nyimbo za watu na kutokuwa na kipaji kutoka moyoni, ndiyo maana unakuta akitoka hapo anapotea. Unakuta ametoa wimbo mmoja tu baada ya hapo mashabiki wanamsahau tofauti na wale ambao wanaishia tano bora au kumi bora.
“Ni vyema wasanii hao wangekuwa wakitumia vizuri ushindi ambao wanauÂpata katika kujiendeleza na siyo kupata jina tu la kuwa mshindi wa shindano hilo. Muhimu ni kuwa na kipaji, si kuimba wimbo wa msanii fulani anayekubalika
SWAGGAZ: Unatoa neno gani kwa waandaji wa shindano la Bongo Star Search?
KALA: Ningependa kuwaomba waandaji wa shindano hilo washiriki wanapofika Top 10, wawapeleke wasanii wao studio warekodi nyimbo zao ili waweze kuwajaji kupita nyimbo hizo na siyo kuingia fainali na nyimbo za kukopi.
Lakini pia wangeweka mkazo kwa kuwashauri washiriki waimbe nyimbo zao wenyewe zaidi kuliko za wengine ili kujizoesha katika kuimba na kutunga, hii ingewasaidia kutokupotea kwa urahisi
baadaye.
 SWAGGAZ: Unaizungumziaje Hip Hop ya sasa na ya zamani?
 KALA: Kwanza kabisa siipendi Hip Hop ya sasa kwasababu imepoteza ladha na mwelekeo tofauti na ya zamani. Zamani watu walikuwa wakiimba vitu bila kuficha lakini siku hizi tumekuwa tukiilainisha Hip Hop sana, jambo linaloipotezea ladha na uhalisi wake kama Hip Hop.
Hiyo inanisababisha niwe nasikiliza zaidi ngoma za Hip Hop za zamani amÂbazo kwa kweli zinaniongezea hamasa ya kubuni vitu vipya vyenye msisimko, vinavyosikilizika na mashabiki wangu.
 SWAGGAZ: Katika ngoma zako, ni wimbo gani unaoukubali zaidi kuliko nyingine zote?
 KALA: Wimbo ulionitoa kimasoÂmaso katika tasnia hii ni Wimbo wa Taifa kwa sababu niliuimba bila uoga, ukanifanya nijulikane sana. Lakini pia naukubali zaidi kwa sababu nilifikiÂsha ujumbe kwa jamii bila kupinÂdisha kwani niligusa kila sehemu iliyokuwa na upungufu.
 SWAGGAZ: Unazungumziaje bifu za wasanii kupitia mitandao ya kijamii?
KALA: Sipendi bifu zisizokuwa na msingi kwani zinafanya mtu ushindwe kufanya vitu vya maana, kiukweli nachukia sana mabifu. Lakini wenzetu nje wana mabifu yenye kujenga, utakuta wanatengeneza bifu lakini mwisho wake wasanii wenyewe wananufaika, siyo kama huku kwetu.
 SWAGGAZ: Vipi kuhusu changamoto?
 KALA: Kiukweli changamoto ni nyingi ila kubwa ni mabadiliko ya muziki, kwani kuna kipindi unakuta soko linabadilika kuÂtokana na muziki, hivyo unaona ni bora ubadilike kwa kufuata upepo unapokÂwenda.
 SWAGGAZ: Hujawahi kufikiria kufanya video nje ya nchi kama wanavyofanya wasanii wengine?
 KALA: Mimi nikitaka kufanya kazi nje nchi basi labda ujue ni Marekani tena na msanii mkubwa kama Jay Z, vinginevyo bora nibaki tu hapahapa nyumbani. Napenda kufanya kazi zangu hapahapa Tanzania ili kuitangaza vyema nchi yetu.
Kuna mazingira mazuri sana ya kuyaÂtangaza ambayo hata nchi za wenzetu hakuna, hilo nitalionyesha katika video yangu hii mpya ya Malkia ambayo imefaniÂkiwa kutangaza mazingira yetu vizuri