MSANII wa miondoko ya Taarabu nchini Khadija Omar ‘Khadija Kopa’ amesema ana furaha kutimiza miaka 25 katika tasnia hiyo hivyo atawashukuru mashabiki wake kwenye tamasha la Mitikisiko ya Pwani litakalofika leo usiku katika Ukumbi wa Dar Live.
Akichonga na Swaggaz, Khadija alisema mashabiki wa muziki wa Taarabu waliopo jijini Dar es Salaam na vitongoji
vyake wajumuike naye ili washereherekee pamoja kwenye tamasha hilo kubwa la Taarabu nchini.
“Nashukuru kupata fursa hii kwani ni heshima ya pekee kwa kutambua umuhimu wa uwepo wangu katika kushiriki
tamasha hilo, nawaomba mashabiki wangu jamani msikose,” alisema.
Mbali na Kopa wengine watakaotumbuiza ni Jahazi Modern Taarab, Wakaliwao, Kopa Kopa, Dogo Jack na mkali wa
Singeli, Msagasumu.