Kala Jeremiah atamani kuwa baba mchungaji

Jeremiah Masanja ‘Kala Jeremiah’
 Jeremiah Masanja ‘Kala Jeremiah’
Jeremiah Masanja ‘Kala Jeremiah’

NA THERESIA GASPER,

MSANII wa miondoko ya hip hop, Jeremiah Masanja ‘Kala Jeremiah’, ameweka wazi kwamba kama asingekuwa msanii angekuwa mchungaji kwa kuwa anaipenda kazi hiyo kwa muda mrefu.

Akizungumza na MTANZANIA jana,  Kala alisema siku zote hupendelea kufanya kazi inayosaidia jamii ndiyo maana mashairi yake yanailenga jamii na kufundisha.

“Awali nilikuwa na ndoto ya kuwa baba mchungaji lakini hapo baadaye nilibadilisha na kuingia katika muziki wa kizazi kipya, kazi ambayo naifanya hadi leo,” alisema msanii huyo anayetamba na video ya ‘Malkia’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here