23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Waliokosa tuzo za ZIFF mwaka jana kukabidhiwa mwaka huu

zix

NA FESTO POLEA

WAANDAAJI wa Tamasha la 19 la Kimataifa la Filamu (ZIFF), wamesema wale wote walioshinda tuzo za mwaka jana lakini hawakukabidhiwa tuzo zao kutokana na sababu mbalimbali watakabidhiwa katika tamasha la mwaka huu linalotarajiwa kuanza kesho visiwani Zanzibar.

Baadhi ya wasanii walioshinda na hawakukabidhiwa tuzo zao ni pamoja na Mtanzania anayeishi Marekani, Honeymoon Mohammed, aliyeshinda tuzo mbili ikiwemo mwongozaji bora wa filamu na filamu yenye picha bora kupitia filamu yake ya ‘Daddy’s wedding’.

Meneja wa Tamasha hilo, Daniel Nyalusi, aliliambia MTANZANIA kwamba washindi hao watakabidhiwa tuzo zao katika tamasha la mwaka huu.

Alisema tuzo hizo zilishindikana kukabidhiwa kwa walengwa kwa kuwa zilivunjika zikiwa zinasafirishwa kwenye ndege.

“Ni kweli mwaka jana kulitokea tatizo la baadhi ya tuzo zilizokuwa zinatoka nje kwani zilivunjika zikiwa katika ndege hivyo ikashindikana kuwakabidhi walengwa lakini tuliwaomba radhi na tuzo zao zimetengenezwa upya na tunataraji katika tamasha la mwaka huu tukawakabidhi tuzo zao,” alieleza Nyalusi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles