23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KADINDA AKANUSHA KUGOMBANA NA WEMA

Na ESTHER GEORGE


wema-sepetuMBUNIFU wa mavazi nchini, Martin Kadinda, amesema hana ugomvi wowote na nyota wa filamu, Wema Sepetu, kama watu wanavyodai.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kadinda alisema watu wamezoea kukaa na kutengeneza mambo ambayo hayapo, yeye ni meneja wa Wema na ataendelea kufanya naye kazi kama kawaida.

“Watu wamezoea kuzusha kila kukicha, kwa upande wangu sijawahi kugombana na Wema, ila kuna watu wana uwezo mkubwa wa kutengeneza habari ambazo hazina ukweli wowote hasa katika mitandao ya kijamii,” alisema Kadinda.

Mbunifu huyo aliongeza kuwa kwa sasa yuko bize na kazi zake za kubuni mavazi kama vile ya harusi ambayo yanamfanya azidi kuwa maarufu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles