NETANYAHU AIPINGA HOTUBA YA KERRY KUHUSU MAKAZI

0
682
Benjamin Netanyahu

YERUSALEM, ISRAEL


Political Leaders Address Annual AIPAC Policy ConferenceWAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameshutumu hotuba ya Waziri wa Wambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, akidai inaikosoa Israel kiuonevu.

Netanyahu amesema Kerry amekuwa akikosoa sana mpango wa Israel wa kupanua makazi yao katika ardhi ya Wapalestina, lakini hakosoi vya kutosha uchochezi unaofanywa na Wapalestina.

Kerry alikuwa ameutetea uamuzi wa nchi yake wa kuliwezesha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha uamuzi wa wiki iliyopita uliotangaza ujenzi wa makazi ya Wayahudi katika ardhi ya Wapalestina kuwa ni kitendo kinachokiuka sheria za kimataifa.

Kerry alisema hatua hiyo ina nia ya kulinda uamuzi wa kuwapo kwa mataifa mawili ili kuzuia hatari ambayo ingeweza kutokea.

Alisema bila ya usalama wa Israel na uwepo wa Palestina, Israel hakutakuwa na amani kamili.

Lakini hata hivyo, Netanyahu ameeleza kuvunjwa moyo na hotuba hiyo, ambayo ameielezea kuwa si sawa.

Alisema ukweli ni kwamba Wapalestina wamekataa kukubali uwepo wa Israel.

Kwa upande wake, Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas alisema atakuwa tayari kurudi katika mazungumzo pale tu Israel itakapoacha kujenga makazi mapya ya wananchi wake katika eneo la Wapalestina.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here