27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

 Kada CCM kizimbani kwa kughushi cheti cha ndoa

Na MWANDISHI WETU DAR ES SALAAM


ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Nora Waziri maarufu kama Nora Mzeru, jana alifikishwa   katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akidaiwa kughushi cheti cha ndoa.

Ilidaiwa   na Wakili wa Serikali, Ester Kyara, mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule  kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kwa kugushi cheti cha ndoa   namba ya usajili 00040078 kwa nia ya kuonyesha kwamba alifunga ndoa na Silvanus Mzeru.

Wakili   alidai   katika siku isiyojulikana Dar es Salaam, kwa nia ya kudanganya, mshitakiwa alighushi cheti hicho kuonyesha kuwa alifunga ndoa na Mzeru Februari 4,1995 katika Kanisa Katoliki la Mburahati wakati   si kweli.

Mshtakiwa   alikana mashitaka na Hakimu Haule alitoa masharti ya dhamana ambapo mshitakiwa alitakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni mbili.

Mshtakiwa aliachiwa huru kwa dhamana hadi Novemba 21 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles