25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Kabwe amshangaa Makonda, akana tuhuma

WILSON KABWENA JOHN MADUHU, MWANZA

MKURUGENZI wa Jiji la Dar es Salaam aliyesimamishwa kazi, Wilson Kabwe amesema hahusiki na tuhuma zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kabwe alitoa kauli hiyo, baada ya kutafutwa na MTANZANIA ili kupata maoni yake baada ya Rais Dk. John Magufuli kutangaza kumsimamisha kazi.

Kabwe alisema tuhuma zinazoelekezwa kwake ni za uongo na kwamba zimelenga kumchafua mbele ya Rais Magufuli.

Mkurugenzi huyo alishangaa kuhusishwa na tuhuma hizo na kusema kuwa, wakati sheria ndogo zinapitishwa na uongozi wa Jiji la Da es salaam yeye hakuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo.

“Sihusiki na mikataba inayosemwa, huu ni uongo mtupu, Makonda ametoa taarifa za uongo kwa Rais.

“Tuhuma zinazoelekezwa kwangu ni za uongo na zimelenga kunichafua mbele ya Rais, nasisitiza tena hakuna mkataba wowote ambao ofisi yangu iliingia kwa nia ya kupoteza mapato ya Serikali,” alisema Kabwe.

Kuhusu mkataba wa ukusanyaji mapato mwaka wa 2004, Kabwe alisema madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam walipitisha sheria ndogo ambayo iliruhusu kila basi katika Kituo cha Mabasi cha Ubungo kulipa Sh 200.

Alisema mwaka 2009, yalipelekwa mapendekezo ya kupandisha kiwango hicho hadi Sh 500, lakini madiwani walikataa kupandisha kwa madai kuwa wakati huo ‘stendi’ ilikuwa imevunjwa.

“Madiwani waligoma kupitisha kiwango hiki, kwa madai stendi imevunjwa, kama wangepandisha ingeleta usumbufu kwa wananchi, wakakataa na muhutasari wa kikao upo.

“Hiki kinachodaiwa kupotea na Makonda kimepotea kutoka wapi?… huu ni upotoshaji wa wazi, hizo Sh bilioni 3 anazosema zimepotea kutoka wapi na zilizchukuliwa na nani, ikumbukwe wakati wa kupitisha hizi sheria mimi sikuwa Mkurugenzi wa Jiji,” alisema.

Alisema ameshtushwa na taarifa za Makonda kuwa walikuwa wakitoza Sh 5,000, kwa kila basi, badala ya Sh 200 zilizopo kwa mujibu wa sheria.

 

KUPUMZIKA

Alisema kutokana na hali ya afya kutokuwa nzuri, Desemba mwaka jana aliomba kustaafu utumishi wa umma na kuandika barua kwa Rais ili aendelee na matibabu.

Alisema tangu aandike barua hiyo, hajawahi kujibiwa na kusisitiza kuwa anamheshimu Rais Magufuli na anaamini atatenda haki baada ya vyombo husika kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles