31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Takukuru: Tutamfikisha Lugumi kortini

saidNA PATRICIA KIMELEMETA, DAR ES SALAAM

JALADA la mkataba tata wa Kampuni ya Lugumi Enterprises na jeshi la polisi limetua mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) kwa ajili uchunguzi zaidi.

Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa takukuru, Tunu Mleli alisema kuwa, jalada ya uchungizi dhidi ya kampuni hiyo liko mikononi mwa takukuru ambapo wakimalisha watawasilisha kwenye mamlaka nyingine za kisheria kwa ajili ya hatua zaidi.

“Tayari tumeanza kazi ya uchunguzi wa kampuni ya Lugumi na jeshi la polisi… ikiwa tutamaliza, tutawasilisha mahakamani kwa hatua nyingine za sheria.

“Lakini kwa sasa siwezi kulizungumzia suala hilo kwa undani kwa sababu tayari limeanza kufanyiwa kazi,” alisema, Tunu.

Alisema, Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 37(1) hakiruhusu
kuzungumzia masuala yanayochunguzwa mpaka yatakapokamilika.

Kampuni hiyo inadaiwa kuingia mkataba na jeshi la polisi mwaka 2011 ambako ilipewa zabuni ya kufunga
mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya polisi 108 nchini kwa gharama ya Sh bilioni 37.

Lakini hadi sasa, kampuni hiyo imefunga mashine hizo katika vituo 14 tu katika jiji la Dar es Salaam huku kamuni tayari imekwisha kulipwa Sh bilioni 34 ambazo ni na asilimia 99 ya fedha zote.

Naye Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai(DCI), Diwani Athuman alisema ofisi yake imeiachia Takukuru kufanya
uchunguzi kuhusiana na mkataba wa Lugumi kwa sababu ina mamlaka ya sheria kufanya hivyo.

“Suala la Lugumi tumewaachia Takukuru wafanye uchunguzi kwa sababu wana mamlaka ya sheria ya
kufanya hivyo na sisi tunaendelea kufanya uchunguzi wa mambo mengine yaliyojitokeza na yanayoendelea
kujitokeza,”alisema Athuman.

Alisema hakuna jalada la makosa ya jinai ambalo litapita bila kufanyiwa uchunguzi na ofisi yake, lakini suala
la Lugumi limehusisha na masuala ya rushwa, jambo ambalo limeifanya kuiachia Takukuru kufanya uchunguzi.

Juzi, wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni walidai watasimamia suala hilo kuhakikisha umma unapata ukweli wa suala hilo.

Waziri kivuli na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema taarifa walizonazo zinaonyesha suala hilo linawahusisha baadhi ya vigogo serikalini
Alisema Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ina mamlaka kamili ya kufanya mambo yote bila kushurutishwa lakini anashangaa kuona katika suala hilo kamati hiyo imekosa makali.

“Kamati hii imepewa mamlaka kamili ya kusimamia na kushughulikia masuala yote yanayohusu fedha za Serikali na hapa kuna ufisadi wa mabilioni ya fedha, …inawezekana vipi iitishe mkataba halafu iporwe na kamati nyingine?” alisema Lema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles