28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Justin Bieber awaomba radhi mashabiki Uingereza

Justin-BieberLAS VEGAS, Marekani

NYOTA wa muziki wa RnB nchini Marekani, Justin Bieber, amewaomba radhi mashabiki wake nchini Uingereza baada ya kutangaza kusitisha onyesho alilotakiwa kulifanya nchini humo.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 21, alitarajia kufanya onyesho hilo Agosti 28 mwaka huu nchini humo, lakini amesitisha bila kutaja sababu za msingi.

“Naomba radhi kwa mashabiki wangu nchini Uingereza kwa kusitisha kufanya shoo Agosti 28, lakini lazima nitaifanya muda mfupi ujao.

“Nimeona nitumie muda huu kujipanga vizuri ili niweze kuwapa shoo yenye ubora kutokana na ninavyokubalika na idadi kubwa ya mashabiki, hivyo naomba uvumilivu wenu,” alieleza Berber.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles