27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Chegeni ambwaga Waziri Kamani

KamaniNA JOHN MADUHU, MWANZA

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Raphael Chageni, amembwaga Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani katika kura za maoni za kuomba kuteuliwa kuwania ubunge kwenye Jimbo la Busega mkoani Simiyu.

Hatua ya kushindwa kwa Dk. Kamani, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Simiyu, imemfanya aungane na mawaziri na manaibu waziri wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete walioangukia pua katika mbio za kusaka kurejea katika majimbo yao.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku kadhaa za vuta nikuvute zilizosababisha kuibuka kwa vurugu na hata kuporwa kwa nyaraka za matokeo ya kura hizo.

Akimtangaza Dk. Chegeni kuwa mshindi katika mchakato huo wa kura za maoni, Msimamizi wa Uchaguzi huo ambaye pia ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Busega, William Bendeke, kwa niaba ya katibu wa wilaya,  alimtangaza mshindi huku ulinzi ukiwa umeimarishwa, huku pia Mkuu wa Wilaya hiyo, Paul Mzindakaya akishuhudia utangazaji wa matokeo hayo.

Bendeke alimtangaza Dk. Chegeni mshindi kwa kura 13,048 dhidi ya kura 11,829 alizopata Dk. Kamani.

Akizungumza na wananchi waliofika wakati wa kutangazwa kwa matokeo hayo, Dk. Chegeni aliutaka uongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu kutenda haki katika vikao vya uteuzi na kuacha kuminya demokrasia ndani ya chama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles