28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Juma Nature: Wasanii tuna haki tukapige kura

JUMANA VICTORIA PATRICK

MSANII asiyechuja, Juma Kassim ‘Juma Nature’ na mfalme wa muziki wa uswahilini, Selemani Jabir ‘Msaga Sumu’, walikuwa kiburudisho kikubwa katika uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, uliofanyika juzi katika Uwanja wa Jangwani jijini Dar es Salaam.

Baada ya kumaliza kutumbuiza, Juma Nature aliliambia MTANZANIA kwamba maombi yake kwa wasanii wenzake ni kujitokeza kwa wingi kwenda kumpigia kura mgombea wanayemtaka kwa kuwa nao wana haki ya kufanya hivyo.

“Wasanii tuna haki ya kumpigia kampeni na kuchagua tunayeona anatufaa, lakini pia tukubali mabadiliko kama timu za mpira Yanga na Simba zinavyokubali zikifungwa na huku kwenye siasa nako wakifungwa Oktoba 25 wakubali matokeo ili amani ya nchi yetu iweze kuendelea,” alisema Nature.

Wasanii wengine waliokuwa katika uzinduzi huo kumuunga mkono mgombea urais wa umoja huo ni Jacqueline Wolper, Aunt Ezekiel, Barafu, Msaga Sumu, Hadji Adamu, Jimmy Mafufu na Shamsa Ford.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles