Jay Z kujiondoa kwenye Instagram

0
797

Celebrities Attend The Chicago Bulls Vs Brooklyn Nets Playoff GameLOS ANGELES, Marekani

MSANII wa hip hop nchini Marekani, Jay Z, amepanga kujiondoa kwenye mtandao wa Instagram baada ya juzi kuweka picha ya marehemu Michael Jackson, ikikumbuka Agosti 29 ambayo ni siku ya kuzaliwa ya gwiji huyo wa muziki duniani.

Jay Z aliweka picha hiyo akiwa amepiga na gwiji huyo huku akiandika maneno yaliyosomeka: ‘Heri ya kuzaliwa mfalme wa muziki.’

“Hii inaweza kuwa ni picha yangu ya mwanzo na mwisho kuweka kwenye mtandao wa Instagram kwa kuwa sio mpenzi wa kutumia Instagram hivyo naweza kuacha kuutumia kabisa,” aliandika Jay Z huku mkewe, Beyonce akionekana kuzidi kuwa na idadi kubwa ya mashabiki kwenye mtandao huo wanaofikia milioni 44.4.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here