28.7 C
Dar es Salaam
Friday, May 24, 2024

Contact us: [email protected]

Lollipop: Nasaidia wenye vipaji vya kuimba

10NA CHRISTOPHER MSEKENA

MTAYARISHAJI wa muziki anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Bongo Fleva nchini, Goodluck Gozbert maarufu kwa jina la Lollipop, amejitokeza kusaidia wasanii wenye vipaji na uwezo wa kuimba lakini hawana fedha za kurekodia kazi zao.

Lollipop aliyejipatia sifa kupitia wimbo wa ‘Basi Nenda’ wa Mo Music, aliliambia MTANZANIA kwamba, wenye uwezo wapo wengi lakini wanashindwa kurekodi kwa kuwa hawana fedha za kurekodia ndiyo maana amechukua jukumu la kuwasaidia ili aibue vipaji vya wasanii hao.

Mbali na kutengeneza nyimbo nyingi, mtayarishaji huyo pia ni mwanamuziki wa nyimbo za injili na mtunzi wa nyimbo mbalimbali ukiwemo ‘Basi Nenda’ na  ‘Nitazoea’ za Mo Music pamoja na wimbo wa ‘Nivumilie’ wa Baracka Da Prince aliomshirikisha Ruby.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles