25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

JPM: NI AIBU KUNUNUA DAWA NJE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Rais John Magufuli, amesema ni aibu kwa Tanzania kununua dawa za matibabu nje ya nchi kwa asilimia 94  huku asilimia sita pekee zikinunuliwa nchini.

Pamoja na mambo mengine, Rais Magufuli amewataka viongozi wa dini kuhubiri suala la viwanda vya dawa ili nchi itoke katika ununuzi ya dawa hizo nje ya nchi.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu Machi 26, wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari 181 ya kusambaza dawa ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

“Niwaombe Watanzania wanaojua kuhubiri vizuri wahubiri kuwa tunapoteza bilioni 500 kila mwaka kununulia madawa na vifaa kutoka nje wakati fedha hizo zingebaki hapa na tukafanya vizuri.

“Nimeangalia vifaa vya kina mama lakini nilipoangalia boksi ni pamba tena kutoka China,” amesema.

Hata hivyo, Rais Magufuli ameshangazwa na hatua ya kununua mabomba ya sindano nje wakati Tanzania ina viwanda vya kutengeneza bidhaa za plastiki.

“Tanzania tuna wasomi wengi kwanini tushindwe hata kutengeneza mabomba ya sindano badala yake tunaagiza kutoka nje, tunatengeneza vifaa vya plastiki tunashindwaje kutengeneza mabomba,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles