24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MAKINDA AWAFUNDA WANAWAKE

Na JOHANES RESPICHIUS-DAR ES SALAAM


SPIKA Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda amewataka wanawake nchini kuwashirikisha wanaume katika harakati za kuleta usawa wa kijinsia.

Wito huo aliutoa jana katika warsha ya Uongozi wa Kijinsia kwa Madiwani wanawake wa Dar es Salaam iliyoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) kwa lengo la kuwaongezea uwezo katika utoaji wa huduma kwa jamii.

Aliwataka viongozi hao kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana na wanaume ili kufanikisha lengo la kuleta usawa bila kujali vyama wanakotoka.

“Ikiwa tunahitaji kufikia usawa wa kijinsia lazima wanawake tuwe na umoja bila kujali vyama, kabila au dini zetu lakini sisi peke yetu hatuwezi kwasababu kwenye vyombo vya maamuzi wengi ni wanaume hivyo ni muhimu sana kuwashirikisha ili kutimiza malengo yetu,” alisema Makinda

Kwa upande wake,  Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Chadema), alisema kupitia marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ambayo yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni yamezingatia usawa wa kijinsia.

“Kama tutafanikiwa kuwa na 50/50 kwenye vyama vyetu vya siasa naamini itakuwa rahisi kwenye upande wa Serikali kutekeleza sera hii maana changamoto bado ni kubwa. Mfano kwenye Bunge, kama kusingekuwa na nafasi za viti maalum tungekuwa na wabunge 26 ambao ndiyo wenye majimbo,” alisema Lyimo.

Aidha aliwataka madiwani hao kuwa jasiri katika kupambana na changamoto wanazokutana nazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles