27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

JPM mgeni rasmi mashindano ya Qur-an

Brighiter Masaki

Rais Dk John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano makubwa zaidi ya Qur-an tukufu Afrika 2019 yatakayofanyika Mei 19 nchini Tanzania Latina Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mashindano hayo yatafanyika nchi zaidi ya 20 ikiwemo Tanzania, Saud Arabi, Nigeria, Sudan, Canada, Comoro, Ghana na Ethiopia.

Mashindano hayo ya 20 kufanyika yatakuwa na washiriki 20 na mshindi atajinyakulia Sh milioni 20 za Kitanzania.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mashindano hayo, Sheikh Nurdeen Kishk, amesema mashindano hayo yameshafanyika kwa haute za Hawaii katika nchi washirika na Mei 19 ndiyo yatahitimishwa katika jijini Dar Es Salaam.

“Mashindano haya kwa mwaka huu yatafanyika hapa nchini na mgeni rasmi tunatarajia awe Rais wetu Dk John Magufuli. Katika mashindano hayo kutakuwa na mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka 12 anayeitwa Summaya Juma aliyewashinda wanaume 21 lakini Tanzania itawakilishwa na washiriki watatu wawili kutoka Zanzibar na mmoja kutoka bara” amesema Shekh Kishk.

Shekh Kishk ameongeza kwamba mashindano hayo yamegawanyika katika vipengele vitatu, kitaifa yaani Tanzania ambapo mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12, Sumayya Juma ndiye aliyeibuka mshindi kwa kuwashinda wanaume 21 sehemu ya pili ni Afrika Mashariki na yatatu ni Dunia ambapo nchi zisizopungua 30 zitashiriki.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lianiva amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi katika kupokea ugeni huo mkubwa wa nchi 20.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles