27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

JPM: Chapeni kazi, msiogope kufanya maamuzi

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli amewataka Mawaziri kutoogopa kufanya maamuzi kwa  kuogopa kufanya uamuzi mabaya.

Akizungumza leo, Jumatano, Desemba 9, Ikulu Chamwino jijini Dodoma mara baada ya kuwaapisha mawaziri 21 na manaibu waziri 22, Rais Magufuli amesema sasa mawaziri wanatakiwa kufanya maamuzi bila kuogopa kukosea.

“Ni vizuri ukafanye uamuzi mbaya kuliko kutokufanya uamuzi, unashindwa kutoa uamuzi kwasababu hutaki uonekane mbaya, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita  miradi ya maji zaidi ya  1,400  imekamilika, kwa hiyo mkafanye kazi, kafanyeni uamuzi hasa unaohusu maslahi ya taifa”, amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewataka mawaziri na viongozi wa Serikali  kuzingatia uadilifu na kuhakikisha kuwa maagizo na maelekezo ya Serikali yanafuata utaratibu.

“Ndani ya Serikali sasa hivi kuna ugonjwa mmoja wa ajabu, kwamba hata mawasiliano yanatumwa kwenye ‘group za WhatsApp, barua nyingine ni za siri na zinaishia kuvuja. Tuzingatie maadili ya viapo vyetu na tufanye kazi zetu kwa uadilifu mkubwa, Serikali hufanya kazi kwa maandishi”, amesisitiza Rais Magufuli.

Kuhusu somo la historia, Rais Magufuli ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha kuwa somo hilo linakuwa somo la lazima kufundishwa mashuleni ili wanafunzi waweze kujua historia ya nchi yao.

“Nataka wanafunzi wetu wafundishwe historia ya Tanzania na hii itasaidia kujenga uzalendo, vijana hawajui historia ya nchi yetu, inawezekana masomo haya yatasaidia kujua jinsi wageni walivyokuja wakadanganya wazee wetu”, alisisitiza Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amezungumzia changamoto zilizopo katika sekta mbalimbali ikiwemo matumizi mabya ya fedha za umma ambapo alimtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kufanya uchunguzi wa matumizi mabaya ya fedha yaliyofanywa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kununua gari la gharama ya zaidi ya Sh milioni 400.

Halikadhalika, Rais Magufuli alisema kuwa  katika kipindi cha miaka mitano iliyopita vijiji 9,880 vilipata umeme na katika kipindi cha miaka mitano ijayo vijiji 2,338, vilivyobaki pia vipate umeme, sambamba na kuanza mradi wa uzalishaji megawati 350  za umeme wa maji mkoani Njombe zitakazoingizwa kwenye Gridi ya Taifa.

Vilevile, Rais Magufuli amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa kuhakikisha kero za wasanii na wanamichezo  zinapatiwa ufumbuzi ikiwemo kusaidia wasanii kupata haki zao.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan aliwataka mawaziri  kafanya kazi kwa bidii, ili kutimiza matumaini ya  wananchi  katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

Naye, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema kuwa mawaziri, wameapa kumsaidia mhe. Rais kazi na jukumu kubwa  ni kufanya kazi kwa kuwatumikia watanzania. “Tunahitaji kuona matokeo ya kazi maana miongozo tayari tunayo. Twende tukachape kazi”, amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Mawaziri walioapoishwa

Upande wa Mawaziri Rais Magufuli amewaapisha, Wizara ya Maji- Juma Aweso, William Lukuvi- Wizara ya Ardhi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Innocent Bashungwa, Wizara ya Afya- Dk. Dorothy Gwajima, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa- Elias Kwandikwa, Utumishi na Utawala Bora- Kapten John Mkuchika,  Ofisi ya Waziri Mkuu, sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu- Jenista Mhagama,Ofisi ya Rais Uwekezaji- Profesa Kitila Mkumbo na Dk. Mwigulu Nchemba(Wizara ya Katiba na Sheria).

Wengine ni Dk. Mwigulu Nchemba wa Katiba na Sheria, Wizara ya Elimu- Profesa Joyce Ndalichako,Wizara ya Mifugo na Uvuvi- Mashimba Ndaki, Wizara ya Maliasili na Utalii- Dk Damas Ndumbaro, Tamisemi- Suleiman Jafo, Wizara ya Nishati- Dk Medard Kalemani,Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi- Dk Leonard Chamuriho, Wizara ya Kilimo- Profesa Adolf Mkenda,Wizara ya Madini- Doto Biteko,Wizara ya Viwanda na Biashara- Godfrey Mwambe, Wizara ya Mambo ya Ndani- George Simbachawene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira)- Ummy Mwalimu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Dk Faustine Ndugulile.

Manaibu

Wizara ya Viwanda na Biashara- Kigae Silaoneka, Wizara wa Ardhi- Angelina Mabula, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira- Patrobas Katambi, Wizara ya Mambo ya Ndani- Hamis Hamza Hamisi, Wizara ya Fedha- Mwanaida Ali Khamis, Wizara ya Elimu- Kipanga Juma Omar, Tamisemi- Dk Festo Ndugange, Wizara ya Nishati- Stephen Byabato, Menejimenti Utumishi wa Umma- John Ndejembi, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Kundo Mathew, Wizara ya Mifugo- Pauline Gekul.

mbali na hao pia kuna naibu wizara ya Madini- Ndulane Kumba, Wizara ya Ujenzi- Godfrey Kasekenya, Ofisi ya Waziri Mkuu wenye ulemavu- Ummy Ndelinanga, Wizara ya Maji- Maryprisca Mahundi, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Abdallah Ulega, Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira)- Mwita Waitara, Wizara ya Mambo ya Nje- William Olenasha,Wizara ya Maliasili na Utalii- Mary Masanja, Ofisi ya rais Tamisemi- David Silinde, Wizara ya Kilimo- Hussein Bashe,  Wizara ya Katiba, Sheria- Pinda Mizengo na Wizara ya Afya- Dk Godwin Mollel.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles