27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

RC Kunenge akoshwa na kiwanda cha kisasa cha nyama Kibaha

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge ametembelea kiwanda cha kisasa cha chinjaji na usindikaji wa Nyama cha Tan Choice kilichopo Soga Wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu utakaotumika kuboresha machinjio ya kisasa Vingunguti.

Katika ziara hiyo RC Kunenge ameambatana na Watendaji kutoka Manispaa ya Ilala, Mkurugenzi wa NHC na Watendaji wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kujionea hatua zote za uchinjaji wa Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo kuanzia hatua ya Kwanza Hadi ya mwisho.

Akizungumza Katika ziara hiyo RC Kunenge ameonyesha kuridhishwa na namna kiwanda hicho kinazalisha nyama kwa viwango vya kimataifa jambo linalopelekea asilimia 80 ya nyama inayozalishwa Kiwandani hapo kuuzwa nje ya nchi.

Aidha RC Kunenge amepongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kutafsiri kwa Vitendo ndoto ya Rais Dk. John Magufuli ya Tanzania ya Viwanda jambo lililowezesha kutoa ajira na kuchangia ukuaji wa uchumi.

Hata hivyo RC Kunenge amesema kiwanda hicho pia kitasaidia wafugaji kutoka mikoa mbalimbali nchini kupata soko la uhakika la kuuza mifugo yao kwa bei yenye tija.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Rashid Abdilah amesema kwa Sasa kiasi kikubwa Cha nyama nayozalisha wanaiuza kwenye mataifa ya Falme za kiarabu Kama Oman, Qatar na Kuwait na kueleza kuwa mahitaji ya nyama nje ya nchi bado ni makubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles