25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

JPM azitaka nchi wanachama SADC kuipa kipaumbele teknolojia ya viwanda

Anna Potinus, Dar es Salaam

Rais John Magufuli amewataka Wanachama wa nchi za SADC kuweka kipaumbele kwenye teknolojia ya viwanda ndani ya Afrika na kuweka utaratibu wa kuuziana malighafi na bidhaa nyingine miongoni mwa nchi hizo ili kukuza mitaji na kuendeleza viwanda ndani ya jumuiya hiyo kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya nne ya wiki ya viwanda na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC), jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 5, Rais Magufuli amesema licha ya umuhimu wa viwanda katika maendeleo ya nchi hizo mchango wa sekta ya viwanda katika nchi nyingi za Afrika na za SADC bado ni mdogo.

“Sekta hii inachangia wastani wa asilimia 10 tu ya pato la taifa na katika jumuiya yetu ya SADC inachangia asilimia 11 pekee.

“Nchi za Afrika zimebaki kuwa wazalishaji wa nguvu kazi kwa ajili ya mataifa yenye viwanda, sisi sote ni mashahidi wa vijana wetu wengi wanaotafuta mbinu za kuikimbia Afrika kwenda Marekani hata kwa kuhatarisha maisha yao.

“Mara nyingi wanunuzi wa bidhaa ghafi ndio waamuzi wa bei kwasababu wasipozinunua sisi hatuna pa kuzipeleka, mwenendo huu ndio uliwadidimiza wakulima wetu kutokana na kutotabirika kwa bei,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema kwa upande mwingine nchi za SADC zimeendelea kuwa waagizaji wa bidhaa za viwandani kutoka nje na bidhaa hizo zinazotokana na malighafi zetu huuzwa kwa bei kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles