23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli ahimiza wanachama SADC kuondoa vikwazo sekta ya viwanda

Anna Potinus, Dar es Salaam

Rais John Magufuli, amewataka wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kuhakikisha wanaondoa vikwazo vyote vinavyochangia kurudisha nyuma maendeleo ya sekta ya viwanda ndani ya jumuiya hiyo ili kurahisisha biashara ya viwanda katika nchi za Afrika.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Agosti 5, alipokuwa akifungua maonesho ya nne ya wiki ya viwanda na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC), jijini Dar es Salaam.

“Tushugulikie vikwazo vyote vinavyochelewasha maendeleo ya sekta ya viwanda, ndani ya SADC tunawekeana vikwazo ambavyo havirahisishi viashara miongoni mwetu, katika mataifa yetu tuna utitiri wa taasisi za udhibiti, utitiri wa kodi, urasimu, vikwazo vya mipakani hivyo hivi vyote tunapaswa kuvitoa ili urahisishe biashara ya viwanda katika nchi zetu,” amesema.

Amesema kukosekana kwa viwanda kunaifanya Afrika iendelee kuwa na uchumi tegemezi na hivyo kuendelea kubaki ndani ya mduara wa umasikini, ambapo amesema mapinduzi ya viwanda ni njia ya lazima kuipitia kuelekea ukombozi wa kweli kiuchumi.

“Historia ya mataifa yaliyoendelea inatufundisha kwamba hakuna njia ya mkato kufikia mapinduzi ya kiuchumi ni lazima tupitie kwenye mapinduzi ya viwanda,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles