25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

JPM AINYOOSHEA KIDOLE UWT

 

Na RAMADHAN HASSAN

-DODOMA

RAIS Dk. John Magufuli ameunyooshea kidole Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) katika maeneo takribani matano tofauti na zaidi akiutaka ubadilike.

Baadhi ya maeneo hayo ni uendeshaji wa Benki ya Wanawake, utoaji au upokeaji wa rushwa, mambo ambayo alisema matokeo yake yalijidhihirisha katika  uchaguzi uliopita.

Akizungumzia Benki ya Wanawake nchini (TWB) na uongozi wake, Rais Magufuli alieleza kusikitishwa na kutowanufaisha wanawake.

Aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa tisa wa Umoja huo, uliofanyika mjini hapa na kuhudhuriwa na mamia ya wanawake, wakiwamo viongozi mbalimbali.

“Benki ya Wanawake haifanyi vizuri, nikiwaficha nitakuwa mnafiki, tangu kuanzishwa na mtaji kupewa na Serikali ‘performance’ yake ni ‘very poor’ na wakopaji wengi ni wanaume.

“Nataka niwaeleze, wala si wanawake wanaokopa pale na ‘interest’ ni kubwa kweli kwa wanawake, sasa unakuwa na benki ya wanawake lakini inawaumiza wanawake.

“Kwa hiyo tutaiangalia vizuri kwa ushindani wa kisasa, hili lazima kina mama niwaeleze, kwani msema kweli mpenzi wa Mungu na katika taratibu za sasa benki ambayo itashindwa kujiendesha inakwenda,” alisisitiza.

Alisema benki yoyote ni lazima ifanye kazi na kisiwe chombo cha kumaliza fedha ambazo zilitakiwa kwenda hospitali au kwenye mikopo.

“Ningefurahi benki hii kila anapokwenda mwanamke bila kuangalia chama chake apate mkopo wenye ‘interest’ ya chini ambao utamwezesha mwanamke.”

Rais Magufuli aliuomba uongozi utakaochaguliwa kulishugulikia jambo hilo ili benki hiyo iweze kuwasaidia wanawake.

ASHANGAA KUKOSA KURA ZA DAR ES SALAAM

Rais Dk. Magufuli alisema licha ya Benki hiyo kuwa Dar es Salaam, lakini Chama Cha Mapinduzi kilikosa kura za wananchi wa Jiji hilo.

“Unaona matawi mengi ya Benki hiyo yapo Dar es Salaam na pamoja na kwamba ipo Dar es Salaam, lakini tulikosa kura za Dar es Salaam,” alisema.

Pengine kutokana na matokeo kama hayo, Rais Magufuli aliwataka wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja huo kuchagua viongozi ambao watakuwa wanajali wanawake na si kujali matumbo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles