24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

JK AONGOZA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA DKT BENDERA

NA OSCAR ASSENGA, KOROGWE


RAIS Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete ameongoza waombolezaji katika mazishi ya aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Dkt
Joel Bendera yaliyofanyika kwenye makaburi ya kanisa la Anglikana Korogwe mkoani Tanga.

Mbali na Rais Kikwete, viongozi wengine wandamizi walioshiriki mazishi hayo ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Suleiman Jaffo, Waziri Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Januari Makamba.

Wakuu wa mikoa, akuu wa wilaya, wabunge na viongozi wa vyama vya siasa na wananachi kutoka mikoa ya Manyara, Morogoro, Dar es Salaam na Tanga

Shughuli za kuuaga mwili huo zilifanyika leo kwenye makazi yake yaliyokuwepo eneo Majengo mji ambapo viongozi mbalimbali walihudhuria wakiwemo mawaziri,wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya na viongozi wa soka nchini wakiongozwa na Rais wa TFF Walace Karia.

Akizungumza katika mazishi hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jaffo alisema serikali imepokea kwa majonzi makubwa msiba huo hasa ukizingatia marehemu alifanya kazi kwa uadilifu mkubwa wakati akitumikia nafasi ya ukuu wa mkoa katika mikoa mbalimbali ikiwemo wa Morogoro na Manyara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles