Jose Chameleone afurahia maisha Marekani

0
1153

joseBAADA ya wasanii wengi kukosa muda wa kuwa karibu na familia zao, msanii tajiri Afrika Mashariki, Jose Chameleone, ameonyesha

mfano bora kwa kusafiri na familia yake ya watoto watatu na mke, Daniella katika ziara ya onyesho lake jijini New York, nchini Marekani.

Mkali huyo wa wimbo wa ‘Tubonge’, alitumia fursa hiyo kuzunguka mitaa mbalimbali ya jiji hilo huku akifurahi na kupiga picha na familia yake kisha kuzituma katika mitandao yake ya kijamii.

Haya wasanii wetu wakati ni huu wa kuimarisha uhusiano wenu kwa kusafiri na mke, mpenzi wako katika ziara
zenu za kimuziki na sanaa nyingine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here