Bima ya Afya yawakabidhi kadi wasanii

0
613

kitimeNA ASIFIWE GEORGE

WASANII wanachama katika mtandao wa wanamuziki Tanzania waliokamilisha taratibu zinazohitajika na mfumo wa Taifa wa Bima ya Afya wamekabidhiliwa kadi za matibabu.

Wasanii hao walikabidhiwa kadi hizo jana, baada ya mafunzo ya uelewa juu ya shughuli za mfuko huo pamoja na faida wanazonufaika nazo wanachama wa mfuko huo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Michael Mhando, alisema huo ni utekelezaji uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha wasanii wanakuwa na bima ya afya ili wawe na uhakika wa kupata matibabu wakati wote.

Naye mwenyekiti wa wanamtandao huo, John Kitime, alisema idadi kubwa ya waliopata elimu hiyo wameshalipia gharama ya kadi, hivyo nao watakabidhiwa kadi zao wakati wowote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here