26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Jokate aahidi kuwapambani Wanawake katika uongozi

*Amshukuru Dk. Samia

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Taifa (UWT), Jokate Mwigelo
amewaomba wanawake wa umoja huo kumpa ushirikiano kwa kile alichosisitiza kwamba unaweza kuwa na nia nzuri ukakosa ushirikiano.

Jokate ameyasema hayo leo Jumatano Oktoba 4, nje ya ofisi za Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya kuchukua fomu ya uteuzi wake kama Katibu Mkuu;

Amesema ana imani kazi yake ndani ya UWT itakuwa nyepesi kutokana na kujipanga vizuri wana mikakati na kwamba kazi yake kubwa ni utekelezaji.

“Mimi ni zao la CCM nimekua kwenye malezi yenu ushirikiano mlionipatia, naomba ushirikiano kwani mafanikio yangu yamechangiwa na nyie,” amesema Jokate.

Amesema wanawake na wasichana washirikiane na wapendane kwa mazuri na mwanamke akigombea katika nafasi mbalimbali wamuunge mkono na wampigie kura.

“Sikutegemea maandalizi haya leo, hii ni ishara tosha kwamba mna imani na mimi, na mimi nawaahidi kuwapa ushirikiano, hutuna budi ya kumsaidia Mwenyekiti wetu, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha nafasi haimponyoki, tunaotakiwa kufanya kazi hiyo ni sisi,” amesema Jokate.

Aidha, amesema moja ya mipango yake nikuhakikisha kuwa chama hicho kinashinda kwenye chaguzi zijazo.

Jokate amesema anatambua waliomsaidia yupo tayari kujifunza na kushauriwa.

Naye Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani, Zainabu Vulu amewataka vijana kufuata nyayo za Jokate kwasababu ni kijana msikivu na mbunifu.

“Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024 nafsi nyingi zinashikwa na wanawake na hivyo wajitokeze na wanategemea mabadiliko makubwa,” amesema Zainabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles