MKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, John Legend, amemshambulia mtoto wa mgombea urais nchini humo, Donald Trump, kwa kudai kwamba baba yake ni mbaguzi.
Legend kupitia akaunti yake ya Twitter, aliandika kwamba, Trump hafai kuwa kiongozi kwa kuwa kuna aina ya watu ambao anapenda kuwaona katika maisha yake, hivyo huo ni ubaguzi kwa kiongozi mkubwa kama huyo.
Hata hivyo, mtoto wa Trump amedai kwamba, Legend anachokifanya sio kizuri kwa kuwa anachafua jina la Trump kwenye mitandao ya kijamii.
“Legend ni msanii mkubwa sana duniani na kitendo anachokifanya kinaweza kusababisha watu wengi kumuunga mkono na kuzidi kuharibu jina la Trump,” aliandika Trump Jr kwenye Twitter.