25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Van der Sar amaliza soka kwa heshima

Barcelona+v+Manchester+United+UEFA+Champions+nxzeJ4sDE9QlNOORDWIJK, UHOLANZI

ALIYEKUWA mlinda mlango namba moja wa klabu ya Manchester United, Van der Sar, amestaafu soka kwa heshima kubwa baada ya kuokoa penalti katika mchezo wa mwisho juzi.

Baada ya kuondoka katika klabu ya Manchester United mwaka 2011, alikuwa nje ya uwanja kwa kudai kwamba amestaafu soka, lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 45, aliomba nafasi ya mwisho kwa ajili ya kuwaaga mashabiki katika klabu ya Noordwijk ya nchini Uholanzi ilipokutana na Jodan Boys kwenye mchezo wa kirafiki.

Van der Sar alipewa nafasi hiyo ya kuwaaga mashabiki ambapo aliisaidia klabu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 huku kipa huyo akiokoa mkwaju wa penalti.

Uongozi wa klabu hiyo ya Noordwijk, umesema kwamba mchezaji huyo ametoa fundisho kwa walinda milango mbalimbali kwa kuwa bado ameonesha kwamba ana uwezo mkubwa na kuwashinda baadhi ya makipa ambao wanapata nafasi kila siku kwenye kikosi.

“Van der Sar ameonesha kwamba bado ana uwezo, ni pongezi kwake kwa kutoa elimu kwa wachezaji wengine, Chama cha Soka Uholanzi kinampongeza mchezaji huyo kwa kumaliza soka lake na kinamtakia maisha mazuri baada ya kustaafu soka,” alisema Katibu mkuu wa klabu hiyo, Peter Vink.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles