27.8 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Ja Rule kukacha muziki kutumbukia kwenye filamu

Ja RuleCALIFORNIA, MAREKANI

RAPA, Jeffrey Atkins ‘Ja Rule’, amedai kuachana na muziki baada ya albamu yake mpya anayotarajia kuiachia wakati wowote ndani ya mwaka huu.

Msanii huyo alisema licha ya muziki kumpa jina kubwa atapumzika kwa kuwa ni muda sahihi kwake kufanya mambo mengine yatakayomwongezea kipato tofauti na muziki.

“Nimefanya muziki kwa kipindi kirefu, natarajia kuachana nao baada ya kuachia albamu yangu mpya mwaka huu, nitaendelea kuupenda muziki lakini kwa sasa ni bora niwapishe wasanii wengine wauendeleze.

“Kuna mambo mengi nitayafanya likiwemo filamu, nimekuwa nikifanya filamu mbalimbali na ninaamini ninaweza kuendelea kwa muda mrefu ila sio muziki,’’ alisema Jarule.

Hata hivyo, aliongeza kwamba atakapoachana na muziki na kuingia katika filamu hataacha kujishughulisha na biashara zake mbalimbali kwa ajili ya kujipatia kipato zaidi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,383FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles