27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

JK ateua DC mpya, ahamisha kumi

Jakaya-Kikwete1Na Aziza Masoud, Dar es Salaam
RAIS Jakaya Kikwete amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa wilaya kwa nia ya kuongeza ufanisi katika uongozi wa wilaya mbalimbali nchini na kumteua Anthony Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Dar es Salaam jana, ilieleza kuwa katika mabadiliko hayo, rais Kikwete amemuhamisha Luteni Edward ole Lenga kutoka Wilaya ya Mkalama mkoani Singida kwenda kuwa mkuu wa Wilaya mpya ya Kyerwa, Mkoa wa Kagera.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Kanali Benedict Kitenga ambaye alifariki dunia Aprili 20, mwaka huu.

Wakuu wengine wa wilaya ambao wamehamishwa ni Elizabeth Mkwasa kutoka Wilaya ya Dodoma kwenda Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Dk. Jasmine Tiisikwa kutoka Wilaya ya Mpwapwa kwenda Wilaya ya Dodoma.
Wengine ni Agnes Hokororo kutoka Wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma kwenda Wilaya ya Tunduru mkoani humo humo na Fadhili Nkurlu kutoka Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera kwenda Wilaya ya Mkalama.
Naye Chande Nalicho amehamishwa kutoka Wilaya ya Tunduru kwenda Wilaya ya Namtumbo wakati Festo Kiswaga amehamishwa kutoka Wilaya ya Mvomero kwenda Misenyi.
Darry Rwegasira amehamishwa kutoka Wilaya ya Karagwe, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Biharamulo mkoani humo humo naye Elias Tarimo amehamishwa kutoka Wilaya ya Biharamulo kwenda Chunya mkoani Mbeya na Deodatus Kinawiro amepelekwa Wilaya ya Karagwe Mkoa wa Kagera kutoka Wilaya ya Chunya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles