27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Jitihada za Serikali kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza

Matende ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza
Matende ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza

Na Ramadhan Libenanga-Morogoro

KUMEKUWA na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukiza yanayotokana na sababu mbalimbali huku kubwa zikitajwa kuchangiwa na mtindo wa maisha.

Hivi sasa idadi kubwa ya Watanzania wanaofika hospitalini wameonekana kuwa na magonjwa ya kisukari, shinikizo la damu pamoja na kuwa na uzito mkubwa huku wataalamu wa afya wakionya kuwa kama watu hawatabadilisha tabia za mwenendo wa maisha yao kuna hatari ya wengi kuugua maradhi hayo.

Serikali inafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha inapunguza vifo vinavyotokana na magonjwa hayo.

Mpango wa Serikali ni kwamba hadi kufikia mwaka 2030 iwe imepunguza theluthi ya vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kukinga, kutibu, kuzingatia afya ya akili na kuboresha huduma za kinga na tiba ya utumiaji wa madawa ya kulevya na pombe.

Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Magreth Mhando, pamoja na rasilimali chache zilizopo Tanzania imepiga hatua katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza licha ya kuongezeka kwa kasi katika nchi zilizoendelea.

Anasema kuwa ulifanyika utafiti kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ambao unaonesha viashiria vya magonjwa yasiyoambukiza kuongezeka.

Anasema idadi ya watu wanaovuta sigara ni asilimia 15.9, wanaokunywa pombe (29.3), wenye uzito kupita kiasi (34.7), shinikizo la damu (25.9) na wagonjwa wa kisukari (9.1).

Naye Kaimu Mkurugenzi Msadizi wa Magonjwa yasiyo kuambukiza kutoka Wizara ya Afya, Shadrack Dusweli, anasema wameweka mikakati kwa kushirikiana na wataalamu wa afya kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Dusweli anasema vitu vinavyosababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni mtindo wa maisha, unywaji pombe, uvutaji wa sigara, ulaji ovyo, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kutofanya mazoezi.

Pia anasema wameweka mikakati ya kupunguza magonjwa hayo kwa kushirikiana na jamii, kuongeza wataalamu, kuteua wataalamu kila mkoa na wilaya na kwamba Desemba 17 mwaka huu watazinduliwa kampeni ya upimaji magonjwa yasiyoambukiza hapa nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles