32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

JINSI VYOMBO VYA PLASTIKI VINAVYOAMBUKIZA SARATANI

NA HERIETH FAUSTINE-DAR ES SALAAM


IMEBAINIKA kuwa vifaa vya plastiki hutengenezwa kwa kemikali zaidi ya 200, hivyo kuwa chanzo cha aina 100 za ugonjwa wa saratani.

Vifaa hivyo vya plastiki ni pamoja na mifuko ya rambo, bakuli, vikombe na vifaa vya kuhifadhia chakula (makontena).

Hayo yalisemwa na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya Marafiki wa Watoto wenye Saratani Tanzania, Walter Miya, wakati wa uhamasishaji wa kupima afya kwa watoto.

 Alisema toka matumizi ya plastiki yazidi kuongezeka nchini, ugonjwa wa saratani nao umeongezeka, hasa kwa upande wa akina mama.

Kwamba ugonjwa wa saratani umekuwa ukiharibu ukuaji wa mfumo wa uzazi, hususani kwa watoto ambao bado kuzaliwa, mabadiliko ya kijenetiki na kushindwa kuona vizuri.

Alisema kupitia utafiti mdogo walioufanya, inaonyesha asilimia 60 za saratani zimesababishwa na matumizi ya vifaa vya plastiki.

“Watu wengi wamekuwa wakitumia vifaa vya plastiki bila kujua madhara yake, ukienda majumbani utakuta wanawake wengi wanachemsha maji na kuyahifadhi katika ndoo za plastiki yakiwa bado ya moto.

“Baada ya muda ukija kuchunguza ile ndoo utakuta ina mabaka mabaka, maana yake imeshatoa kemikali nyingi na kuingia katika yale maji na athari hutoiona kwa muda huu, mpaka ifike miaka 10 au 15 na huwezi kugundua saratani yako imesababishwa na nini,” alisema Miya.

Alisema jamii inapaswa kupunguza matumizi ya plastiki kutokana na madhara yaliyomo katika vifaa hivyo na kuwataka wachemshao maji kusubiri hadi yapoe ndipo wayamimine katika ndoo.

“Kuna vitu vingi ukiviangalia unaweza ukaogopa ila huwezi kuvikimbia, ni kuangalia ni namna gani tunaweza kuvipunguza ili athari ya saratani isizidi kuongezeka.

Alisema hata hivyo wanahitaji sera na sheria dhidi ya matumizi ya plastiki kutokana na kukithiri kwa vifaa hivyo ambavyo vimekuwa vikitengenezwa kila kukicha viwandani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles