KHARTOUM, Sudan
WANAJESHI nchini Sudan leo wamewashikilia baadhi ya vigogo wa Barala za Mawaziri, akiwamo Waziri Mkuu, sambamba na viongozi wa upinzani katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni jaribio la kuipindua Serikali,
Waziri Mkuu, Abdalla Hamdok, alikamatwa na kupelekwa kusikojulikana baada ya kukataa agizo la jeshi kumtaka aunge mkono mapinduzi, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Habari ya Sudan.
Huku ikikumbuka kuwa jaribio la kuipindua Serikali lilifeli mwezi uliopita, hali ya usalama nchini humo imekuwa ya kutilia shaka kutokana na uadui unaotokana na kugombea madaraka kati ya jeshi la vikundi vya kiraia.
Mwaka 2019, jeshi lilimpindua Rais wa muda mrefu, Omar al-Bashir, ambaye aliishia gerezani, lakini bado kumekuwapo na sintofahamu kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka 2023.