26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

JESHI LA MAGEREZA LAFUMULIWA

 

 

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM


 

KAMISHNA  Jenerali wa Jeshi  la Magereza, Phaustine Kasike  amefanya mabadiliko madogo ya kiuongozi kwa wakuu wa magereza wa mikoa na vituo vingine nchini.

Mabadiliko hayo yamewagusa vigogo kadhaa akiwamo aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP), Julius Sang’udi  ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wafungwa na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP), Salum Hussein.

Taarifa iliyotolewa jana na Ofisa Habari wa Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje ilieleza kuwa aliyekuwa Mkuu wa Gereza Mtego wa Simba, Kamishna Msaidizi wa Magereza(ACP), Msepwa Omary amehamishiwa Magereza Mkoa wa Singida kuwa Kaimu Mkuu wa Magereza mkoa huo na nafasi yake inakaimiwa na Mrakibu wa Magereza, Muta Tibalinda.

Katika mabadiliko hayo, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP), John Masunga amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kitengo cha Viwanda vya Jeshi la Magereza huku nafasi yake ikikaimishwa kwa aliyekuwa Mnadhimu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP), Emmanuel Lwinga.

Wengine ni aliyekuwa Boharia Mkuu wa Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP), Afwilile Mwakijungu alihamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mdhibiti Mkuu wa Shirika la Magereza na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP), Goleha Masunzu.

Pia aliyekuwa Ofisa Mwandamizi wa Utawala, Magereza Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP), Benezeth Bisibe amepelekwa kuwa Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mara.

Aliyekuwa Naibu Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), anayeshughulikia taaluma, utafiti na ushauri, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP), Joel Matani anakuwa mkuu wa chuo hicho na nafasi yake imechukuliwa na Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP), Wilington Kahumuza ambaye alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo, akishughulikia manunuzi, fedha na utawala na nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP), Ahmad Seleman.

Wakati huo huo, Kamishna Jenerali wa Magereza amemteua Mrakibu wa Magereza (SP), Amina Kavirondo kuwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Magereza katika kile kilichoelezwa kuwa mabadiliko hayo yanalenga kuboresha utendaji kazi wa jeshi na kuongeza ufanisi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles