23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Jerry Muro aiombea Yanga kwa TB Joshua

jery muro*Ataka ubingwa Ligi Kuu, Shirikisho utue Jangwani

*Wapinzani wao Esperanca wagawa pointi Angola

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

OFISA Habari wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro, amesema ameiombea klabu yake hiyo kwa Nabii maarufu nchini Nigeria, T.B Joshua, alipokwenda nchini humo kwa ajili ya shughuli zake binafsi.

Muro ni mmoja wa Watanzania walioshiriki misa ya Jumapili katika kanisa la nabii huyo maarufu Afrika, ambaye anasifika kwa utabiri wa kweli.

Umaarufu wa TB Joshua ulishika kasi nchini mwaka jana katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba, baada ya waliokua wagombea wa nafasi ya urais, Rais wa sasa, John Magufuli (CCM) na Edward Lowassa (Ukawa) kufika Nigeria kabla ya uchaguzi huo kwa ajili ya maombi.

Mbali na kuwaombea wagombea hao, T.B Joshua siku moja kabla ya kuapishwa Rais wa Awamu ya Tano, Magufuli, Novemba 4 alifika nchini na kupokelewa na Rais huyo ambapo baadaye alikutana Ikulu na Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Baada ya hapo T.B Joshua alikutana na Lowassa ambapo baadaye alifanya misa ya pamoja na familia yake kabla ya kuondoka kurudi Nigeria.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Muro alisema alienda kwa Nabii huyo kwa ajili ya mambo yake binafsi, pia alishiriki ibada iliyofanyika Jumapili iliyopita katika kanisa lake.

“Ilikua Jumapili muhimu kwangu, nilishiriki ibada mbali ya kujiombea na familia yangu niliiombea klabu yangu pendwa ili iweze kufanya vizuri katika michuano ya Ligi Kuu na ile ya kimataifa ikiwemo kuchukua mataji hayo.

“Niliondoka nchini Jumatano Aprili 20 na nimerudi jana (juzi) usiku, kwakweli najisikia ni mtu mwenye amani na sasa nipo Mwanza nimeambatana na timu hapa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Toto,” alisema.

Muro alisema furaha yake ni kuona Yanga inapata mafanikio.

Wakati huo huo, wapinzani wa Yanga katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Sagrada Esperanca, juzi walikiona cha moto kwenye Ligi Kuu ya nchini Angola baada ya kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Interclude.

Kipigo hicho kilitibua maandalizi ya Waangola hao kabla ya kuikabili Yanga Mei 6, mwaka huu kwani kimewafanya washuke kutoka nafasi ya nne hadi ya saba kwa kufikisha pointi 13 wakiwa wameshuka dimbani mara tisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles