STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, amesema msanii mwenzake, Rehema Chalamila (RC), anahitaji kuwa na marafiki sahihi watakaomsaidia katika kipindi hiki kigumu.
Lady Jaydee alisema hayo wakati msanii mwenzake huyo anayedaiwa kurejea kwenye utumwa wa matumizi ya dawa za kulevya alizokuwa akipigania kuziacha alipomtembelea nyumbani kwake hivi karibuni.
“Ray C alikuja kunisalimia nyumbani, kwa kipindi anachopitia sasa ni kigumu anahitaji marafiki sahihi ingawa sikusema kama naweza kumsaidia chochote,” alisema Lady Jaydee.
Hata hivyo, Jaydee aliongeza kwa kumuombea msaada Ray C kwa yeyote mwenye lengo la kumsaidia kwa mchango ama kuwa naye karibu wafanye hivyo huku akisisitiza kwamba asitengwe.