23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Tausi Likokola kusaka warembo nchi nzima

LIKOKOLAGLORY MLAY NA BEATRICE KAIZA

MWANAMITINDO wa kimataifa anayefanyia kazi zake nchini Marekani, Tausi Likokola yupo katika maandalizi ya kutafuta warembo wenye vipaji vya kufanya shughuli za uanamitindo mikoa mbalimbali nchini.

Katika kuhakikisha hayo mrembo huyo ameanzisha African Princess Model Search, itakayokuwa na jukumu la kukusanya warembo kutoka nchi nzima na watakaopatikana watawekwa kambini jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mafunzo maalumu ya uanamitindo.

Mrembo huyo ana vitabu vinne kikiwemo, The African Princess anachotarajia kukitoa Jumamosi hii kingine ni Out of Beauty and Health.

Tausi alisema ameamua kuanzisha mashindano ya wasichana wa Tanzania kwa sababu ameona wengi wao ni wavivu wa kujishughulisha licha ya kuwa na kipaji huamka na kukaa huku wakiwa wamekata tamaa.

“Nikiwapata wasichana hao nitawafundisha kazi anazotakiwa kufanya mrembo na kuachana na uvivu kisha watakaoendana na mafunzo hayo nitabaki nao na kuwatumia katika kazi zangu za mitindo za kimataifa ninazofanya,” alisema Tausi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles