24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Jennifer Lawrence avishwa pete ya Milioni 229

NEW JERSEY, MAREKANI 

STAA wa filamu nchini Marekani, Jennifer Lawrence, amevishwa pete ya uchumba yenye thamani ya dola 100,000, ambazo ni zaidi ya milioni 229 za Kitanzania.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 28, alionekana Jumamosi wiki iliopita akiwa ameivaa kwenye tamasha la Veuve Clicquot Polo Classic event huko New Jersey.Hata hivyo, mrembo huyo hakutana kumuanika mwanaume ambaye amemvisha pete hiyo.

Kabla ya kuvishwa pete hiyo, alikuwa kwenye uhusiano na Cooke Maroney, lakini ilidaiwa kuwa wawili hao wameachana na Maroney amepata mchumba mwingine.

Jennifer ni kati ya wasanii wa filamu ambao wameandika historia, mwaka 2015 hadi 2016 alitajwa kuwa ni msanii ambaye analipwa kiasi kikubwa cha fedha nchini Marekani kwa upande wa wanawake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles