29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Van Dijk ajipa tuzo ya Ballon d’Or

MADRID, HISPANIA

BAADA ya Liverpool kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, beki wa kati wa timu hiyo Virgil van Dijk, anaamini ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya Ballon d’Or msimu huu.

Beki huyo amedai mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi alikuwa na nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo, lakini baada ya Liverpool kuchukua ubingwa msimu huu basi ni wazi Messi hana nafasi hiyo.

Van Dijk raia wa nchini Uholanzi, amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Liverpool tangu aliposajiliwa na timu hiyo Januari 2018. Aliweza kuutengeneza ukuta imara katika safu ya ulinzi ya Liverpool.

Hata hivyo baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu msimu huu, beki huyo alitajwa kuwa mchezaji bora wa msimu huu, hivyo anaamini bado ana nafasi ya kuwa bora kwenye Ballon d’Or na kuandika historia ya kubwa beki bora wa kutwaa tuzo hiyo baada ya mwaka 2006 ambapo ilichukuliwa na Fabio Cannavaro.

“Ninadhani kuwa Messi ni mchezaji bora duniani, alistahili kutwaa Ballon d’Or msimu huu, lakini kwa sasa sifikirii kama atakuwa na nafasi hiyo kwa kuwa tayari Liverpool tumechukua ubingwa.

“Bado Messi atabaki kuwa mchezaji bora duniani hata kama hakuweza kuisaidia timu yake kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa,” alisema beki huyo.

Beki huyo aliongeza kwa kusema, ubingwa huo wa Ligi ya Mabingwa utawaongezea kitu fulani msimu ujao wa Ligi hasa katika kushindana na mabingwa wa Ligi Kuu England, Manchester City.

“Ubingwa una maana kubwa sana kwetu, tunaamini msimu ujao tutakuwa na kitu kipya cha kwenda kukifanya kwenye Ligi Kuu hasa kuleta changamoto kwa wapinzani wetu Manchester City, tunaamini msimu ujao hawatoweza kufanya lolote na tunataka kuendelea kufanya hiki tulichokifanya leo (juzi), katika misimu kadhaa ijayo,” aliongeza beki huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles