27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

Kourtney Kardashian atamani ujauzito

NEW YORK, MAREKANI 

MWANAMITINDO kutoka familia ya Kardashian, Kourtney Kardashian, ameweka wazi kuwa, anatamani kushika ujauzito ili kuongeza ukubwa wa familia yake.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 40, kwa sasa ana jumla ya watoto watatu, lakini amesisitiza kuwa kuongeza watoto ni kitu ambacho anakifikiria kwa sasa.

“Kuwa mama ni kitu ambacho ninakipenda katika maisha yangu, kwa sasa ni mama kwa kuwa nina watoto, lakini bado natamani kuongeza watoto wengine kwa siku za hivi karibuni.

“Kila mmoja amekuwa na mtazamo wake, lakini kwa upande wangu ninajisikia furaha nikiwa na ujauzito, ninaamini siku za hivi karibuni ninaweza kuwa kwenye mpango wa kuongeza watoto,” aliandika mrembo huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles