31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

JECHA AKIRI ZANZIBAR SI SHWARI

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM


 

Jecha Salim JechaMWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha amekiri wazi kwamba siasa zimeharibu utengamano wa wanannchi, huku akiwataka wanasiasa visiwani humo kupunguza jazba ili waijenge nchi yao.

Jecha aliyasema hayo jana katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na Televisheni ya Azam, kilichoongozwa na Mtangazaji mkongwe, Tido Mhando.

Pamoja na mambo mengine, Jecha alisema kutokana na jazba hizo, itachukua muda mrefu kwa Zanzibar kujenga maelewano ya kindugu.

Tido:   Unafikiri nini kifanyike ili Zanzibar iweze kuwa na utulivu na watu kukaa pamoja bila chuki.

Jecha:   Kinachotakiwa watu tupunguze jazba ya kisiasa tukae tukubaliane na tujenge nchi yetu, lakini kutokana na jazba hizi itachukua muda sana katika hili.

Tido:  Unaponambia jazba ya kisiasa nakuelewa lakini kulikuwa na maridhiano ila matokeo ya uchaguzi uliopita yameondoa maridhiano hayo kabisa.

Jecha: Matokeo yaliyopita  hayajaondoa maridhiano kwani  yapo kwenye Katiba lakini utaratibu wake ndio uliovurugika kidogo.

“Na hii jazba  ya kisiasa imesababisha hadi watu hawaendi kuzikana kabisa, ndio imefika hapa tulipo sasa kikubwa waondoe jazba na ndio itatufikisha mbali katika maendeleo ya kujenga nchi.

“Ndugu hawaongei, hawasalimiani, jamii haziabudu pamoja wala haziwi huru, wanaogopa, watu hawafanyi huduma za kijamii hata kwenye gari za abiria watu wanasusiwa hii haipendezi ,’’alisema Jecha.

Aliongeza kwa kuhoji kuwa ni kwa sababu gani mazao ya watu katika visiwa vya Pemba yanaharibiwa hii haijawahi kutokea, nyumba zinachomwa moto, mifugo inauliwa jambo ambalo si ubinadamu.

“Jaziba za kisiasa ndugu hawaongei ni uhasama , mtangazaji uje zanzibar utembee usikie watu wanavyoishi kwa sasa.

Tido :  Huoni  hali hiyo inatokea  kwa sababu kuna hali  ya ung’ang’anizi kwamba upande mmoja unashindwa lakini kila siku hawakubali na wanatumia kila njia kubakia madarakani?

Jecha: Hakuna ung’anganizi, uchaguzi ulifutwa, kila chama kilikuwa huru kupeleka majina na kila chama kilishiriki uchaguzi ulikuwa huru, vyama vyote vilishiriki uchaguzi.

Tido: Inaonekana ulifuta uchaguzi wakati huo ukiwa na hisia kali.

Jecha : Sikuwa na hisia kali  ni uchaguzi wa kawaida na umefuata sheria zote hakuna tatizo sikuwa na tatizo.

Tido: Lakini ni kitendo kipya si jambo la kawaida

Jecha : Uchaguzi wowote unatawalia na sheria na utaratibu na uchaguzi  mwaka 2015 ulikwenda  sawa lakini kulitokea na vitendo vingi ambavyo havikuwa vya kawaida ndio ukasababisha kufutwa kwa uchaguzi huo.

Tido: Ulitaja mambo kadhaa ikiwa ni sababu za kufutwa kwa uchaguzi huo kwa mfano, kufutwa fomu za kura vijana kufanya fujo mtaani, na kutangazwa kwa matokeo mapema.lakini wanasema umetoa sababu hizi wakati watu hawakuyaona huko mitaani na wala hawakuyashuhudia bayana ninyi mkabaini.

Jecha:   Matokeo hayo yalionekana mapema na baadhi ya vyama vilivyoshiriki uchaguzi vililalamikia hayo mambo yaliyosababisha uchaguzi huo kufutwa.

Tido: Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)  inamchanganyiko ya wajumbe wa kutoka vyama mbalimbali vya  siasa hili unalichukuliaje?

Jecha: Hii ni zuri sana lakini ina changamoto hakuna chama kujichukulia mamlaka ndani ya Tume.

Na kuna wakati kuna mambo yanaingizwa kivyama zaidi  hii ndio inakuwa tabu.

Tido : Lakini katika uchaguzi uliopita mambo yalikwenda vizuri,wachunguzi wa mambo walisema hakukuwa na shida, magazeti pia walisema mambo yalikuwa mazuri na hata waangalizi hili lipoje?

Jecha:  Kulikuwa na mambo mengi sana yaliyokuwa na matatizo kwenye uchaguzi huo na nitayatoa mwezi Februari mwaka huu, tayari tumeandaa taarifa bado wakati wake tu kutoka.

Tido : Ulisimamisha uchaguzi lakini watu walijipanga upande pale pale kwenye ukumbi Bwawani, mara wanasikia umeenda kwenye televisheni kutangaza tena peke yako hili lipoje?

Jecha:  Haya yote yataonekana kwenye taarifa ya uchaguzi na si hapa siwezi kusema sasa hivi.

Tido:  Je mlifuata utaratibu?

Jecha:  Utaratibu ulifuatwa na wakati wa matokeo ya Zanzibar hasa Unguja hakukuwa na hitilafu, matatizo yalionekana wazi wazi taarifa zilipoanza kutufikia hasa za kisiwa cha pemba.

Ikaonekana kulikuwa na ukiukwaji mkubwa sana na sio kupiga kura ni baada ya kura zilishapigwa kulitokea na utaratibu mbaya.

‘’Kulitokea utaratibu wa kiufundi ukaharibu matokeo ya kura, ikiwa ni pamoja na urekebishaji wa kasoro kulifanyika mambo ambayo hayakutakiwa kufanyika nje ya uchaguzi,’’alisema Jecha.

Tido: Kuna watu mnadhani walifanya hivyo?

Jecha : Sisi kama tume hatuna watu hao bali Jeshi la Polisi wanayo majina hayo.

Tido: Lakini iweje ielezwe kwamba kura zilizoharibika na vurugu ni za Zanzibar na sio serikali ya Muungano, kwamba kura za  Muungano zilikuwa shwari?

Jecha: Bwana Tido hayo tungeliacha  lakini hisia kali haikuwa kwenye muungano kulikuwa na hisia kubwa  kwenye kura za Zanzibar.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles