23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

PROF. LIPUMBA ANUSURIKA KIPIGO, AKIMBILIA MSIKITINI KUJINUSURU

Na RAMADHAN LIBENANGA- MOROGORO


 

Ibrahim_LipumbaMWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amenusurika kupigwa na vijana wanaoaminika kuwa ni wa Ukawa wakati akitoka kwenye mkutano wa kampeni mjini Morogoro.

Katika vurugu zilizotokea juzi jioni wakati vijana wa Ukawa na kikundi cha ulinzi cha CUF (blue guard) cha Dar es Salaam wakiwa na Profesa  Lipumba walikuwa wakitoka kwenye mikutano ya kampeni maeneo tofauti walipokutana barabarani na kuanza kurushiana maneno na hatimaye kupigana.

Katika vurugu hizo, vijana wa Ukawa waliwazidi wenzao wa blue guard na Profesa Lipumba kulazimika kukimbilia kwenye Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja ili kujinusuru.

MTANZANIA lilishuhudia  ghasia hizo zilizodumu kwa takribani saa moja na nusu ambapo baada ya Profesa Lipumba kukimbilia msikitini hapo, wafuasi wa Ukawa walibaki nje mpaka polisi walipofika na kuwatawanya.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira alikiri kutokea kwa vurugu hizo ambapo alisema wafuasi watatu wa CUF walijeruhiwa.

Alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini walioanzisha vurugu hizo ikiwa ni pamoja na kuweka doria kali katika mikutano ya vyama vya siasa.

Profesa Lipumba hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, baada ya simu yake kutokuwa hewani jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles