25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

JE, SIMU YAKO ITAKOSA HUDUMA YA WHATSAPP 2017?

whatsapp-beta-whatsapp-whatsapp-hidden-features

Na FARAJA MASINDE,

MTANDAO wa kijamii wa WhatsApp ambao mpaka sasa una watumiaji bilioni moja duniani kote, mapema mwezi huu umetangaza habari ambazo huenda zisiwe njema kwa baadhi ya watumiaji wa huduma hiyo ambao vifaa vyao vitakuwa nje ya mfumo wa kisasa unaohitajika.

WhatsApp ambao umejizolea umaarufu mkubwa duniani nakuchukuliwa kama njia ya haraka zaidi ya kupashana taarifa kwa ujumbe wa picha, sauti na hata video mbalimbali umetangaza kufikia uamuzi huo ambao unaweza usifurahiwe na wengi kwa kile ulichoeleza kuwa ni kuboresha zaidi huduma zake.

Mtandao huo umesema kuwa umefikia uamuzi huo wa kusitisha kutoa huduma kwa baadhi ya simu zinazotumia mifumo endeshi (OS) ambayo imepitwa na wakati ili kuweza kuendana na kasi ya ukuaji wa soko la simu duniani na teknolojia kwa ujumla.

Hivyo kwa taarifa hiyo ina maana kuwa kuna baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao mwisho wao wa kutumia huduma hiyo itakuwa ni mwaka huu.

Mabadiliko haya hayajawakumba watumiaji wa simu za Android pekee bali hata wale wanaotumia simu za iPhone ambazo zinatumia mfumo wa uendeshaji wa iOs.

Watumiaji ambao watakosa huduma hii ya WhatsApp ni pamoja na wale wanaotumia simu zinazotumia mfumo huu wa uendeshaji.

Kwa upande wa watumiaji simu za Android watakaoathirika ni wale wanaotumia Version za Android 2.1 na Android 2.2.

Upande wa watumiaji wa simu za Window ni zile zenye mfumo wa Window Phone 7 huku upande wa watumiaji wa simu za iPhone watakaoathiriwa ni wale wenye simu zenye mfumo wa 3GS/iOS6.

Mtandao wa WhatsApp ambao ulianza kupatikana rasmi mwaka 2009 haujaishia hapo, pia umetoa taadhari kwa watumiaji wa simu za Blackberry OS 10 running on BBOS na Nokia S40 running on Symbian S40 ambapo mwisho wa simu hizo kutumia huduma hiyo itakuwa ni Juni 2017.

Kama unakumbuka wakati mtandao huu unaanza kutumika ulianzia kwenye aina mbili za simu za Blackberry na Nokia lakini hicho hakijawa kigezo cha watumiaji wa simu hizo kuendelea kutesa.

“Tunajua kuwa uamuzi huu ni mgumu sana kuuchukua japo tunaamini una tija kubwa kwani utawezesha kuwapatia watu njia bora zaidi ya kuwasiliana na ndugu, jamaa, marafiki,” wamesema WhatsApp.

0653045474.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles