24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

VYUO VYA MAFUTA NA GESI VILIVYOKO CHINA, INDIA

Chuo cha  Lovely Professional University (LPU)
Chuo cha Lovely Professional University (LPU)

Na FARAJA MASINDE,

JITIHADA mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na serikali katika kuhakikisha kuwa azma ya kuwa na Tanzania ya viwanda inafanikiwa.

Ndiyo ni jambo linalowezekana kwani tumeona jitihada kwenye maeneo mbalimbali ikiwamo mkoni Pwani ambao umeonekana kuwa eneo lenye mazingira mazuri ambayo yanafaa kwa uwekezaji.

Hata hivyo msukomo wa viwanda hivyo katika kuhakikisha kuwa vinafanya kazi kwa ufanisi na hata kuleta tija kwa Watanzania ni lazima kuhakisha vinakuwa na nishati ya uhakika ambayo itaviwezesha kufanya shughuli za uzalishaji na unaotakikana.

Eneo hili la nishati ya kuendesha viwanda awali lilikuwa likitazamwa kama sehemu yenye changamoto kubwa zaidi katika kufanikisha uwekezaji huu na hivyo kukuta kwamba likichelewesha wawekezaji wengi kuja kuwekeza hapa nchini.

Kugundulika kwa nishati ya gesi hapa nchini miaka michache iliyopita huko mkoani Mtwara na maeneo mengine ni wazi kuwa itakuwa ni neema kubwa katika kusaidia kukua kwa viwanda vingi na kufanya uzalishaji wa uhakika.

Tumeshuhudia hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na watendaji husika katika kuhakikisha kuwa viwanda  na Watanzania wanapata kutumia tunu hii ambayo ni ya kipekee.

Hata hivyo licha ya kuwapo kwa mkakati huo wa kutumia gesi kwenye viwanda mbalimbali na maeneo mengine hapa nchini, bado kuna changamoto ya wataalamu wa masuala haya ya gesi.

Kuwa na watu watakaokuwa na ujuzi juu ya kuendesha masuala haya ya nishati ya gesi kwenye viwanda na wataalamu wengine watakaokuwa nguzo katika kuhakikisha kuwa gesi hii inatumika ipasavyo bila kuleta athari.

Ni wazi kuwa suala hili la kupata wataalamu wa nishati ya gesi limekuwa changamoto kwani kwasas hapa nchini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ndicho pekee kimeanza kutoa kozi hii licha ya kuwa wanahitajika wataalamu wengi.

Changamoto hiyo ya kukosekana kwa vyuo vya kutosha vinavyotoa kozi za mafuta na gesi imewasukuma wanafunzi wengi kupata shauku ya kutaka kwenda kusaka ujuzi huo nje ya nchi.

Hata hivyo ni wanafunzi wachache ambao ndio wamekuwa wakijua vyuo bora kwenye taaluma hiyo na nchi viliko.

Kutokana na changamoto hiyo ndipo Taasisi ya Global Education Link ikaamua kuwa kiungo kati ya wanafunzi wa kitanzania wanaotaka kwenda kusoma nje ya nchi katika fani hizi za mafuna na gesi.

Ofisa Masoko wa taaisi hiyo, Medard Sotta, anasema kwasasa kuna vyuo ambavyo wanafunzi wa kitanzania wanaweza kwenda kusoma taaluma hiyo nje ya nchi.

Anasema kuna mataifa kama China na India ambayo yamekuwa yakitoa elimu ya mafuta na gesi kupitia vyuo vyake ambavyo ni washirika na mtandao huo hapa nchini.

“Tunajua kuna changamoto ya kupata chuo cha kusoma masuala ya mafuta na gesi hapa nchini, hivyo tumeona tuwe kati ya Watanzania hawa ambao wanataka kutimiza ndoto zao.

“Kama nia ya mwanafunzi ni kubobea kwenye masuala ya mafuta na gesi basi vyuo hivi tutakavyompeleka atatimiza ndoto yake,” anasema Sotta.

Anavitaja baadhi ya vyuo hivyo kuwa ni pamoja na Liaoning Shihua Universty na China Universty of Petroleum vya nchini China pamoja na kile cha Oil& Gas Management na Lovely Professional University (LPU) vya nchini India.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles