29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

JB: MATUTA NGAO YA JAMII YALIFANYA NIJIFICHE TAIFA

Na JESSCA NANGAWE-DAR ES SALAAM

MSANII nguli wa filamu za Bongo na shabiki wa klabu ya Simba, Jacob Steven ‘JB’, amesema wakati timu yake ilipoingia hatua ya matuta katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga  kwenye Uwanja wa Taifa juzi, hakuweza kuangalia na badala yake alijificha.

Akizungumza na MTANZANIA mara baada ya mchezo huo kumalizika, JB alisema pamoja na ushindi walioupata, hakukiamini kikosi chao hivyo alilazimika kujificha kusubiri matokeo.

Alisema kikosi chao ni kizuri, lakini hatua ya matuta ilikua ni kubahatisha kushinda au kushindwa, hivyo alikosa moyo wa kuangalia kilichokuwa kikiendelea.

“Mimi bwana likija suala la penalti ni mipango ya Mungu, hakuna cha fundi, sikuweza kuangalia timu, niliamua kujificha na kusubiri kuona nini kinatokea, baada ya kumalizika niliona Simba wakishangilia nikajua tayari tumewamaliza,” alisema JB.

JB alisema Simba inapaswa kujipanga kikamilifu katika msimu huu mpya, kwani wapinzani wao Yanga  wameonyesha ushindani wa hali ya juu, jambo linaloashiria ubingwa utakavyokuwa mgumu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles