NEW YORK, MAREKANI
MFALME wa muziki wa Hip Hop nchini Marekani, Jay Z, picha yake imeanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii huku akiwa amevaa kofia ya mchezo wa Baseball ikiwa na maneno ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.
Rapa huyo mwenye umri wa miaka 46, kwenye picha hiyo inamwonyesha akiwa mtaani jijini New York akiwa na kofia hiyo yenye maandishi ya kustaafu kujihusisha na madawa hayo.
Mwaka 2013, Jay Z, aliwahi kufanya mahojiano na Vanity Fair, alidai kwamba anaandaa kitabu kitakachokuwa kinapinga watu kujihusisha na madawa ya kulevya.
“Niliwahi kujihusisha na madawa ya kulevya lakini naamini siyo kitu kizuri, nina lengo la kuaandaa kitabu kwa ajili ya kupinga madawa ya kulevya, hivyo kila kitu kipo sawa,” alisema Jay Z.